Breaking




Tuesday, 15 August 2017

MADEE AELEZEA JINSI ALIVYOTENGENEZA VIDEO YA KATUNI



Ukitazama video mpya ya Madee ‘Sikila’ aliyomshirikisha Tekno kutoka Nigeria, utaona utofauti kwani imefanyika kwa mfumo wa katuni (animation).

Madee amesema alifanya hivyo ili kuleta utofauti katika muziki wake na aliyefanya kazi hiyo ni kijana kutoka hapa Tanzania, hata hivyo ameeleza kuwa aina hiyo ya video ni gharama zaidi.

“Kitu ambacho kimenishangaza zaidi hiyo ndiyo mara yake ya kwanza wakati nampa hiyo idea akasema siwezi, sasa mimi nilimuona wapi?, alitengeneza animation moja ya Diamond na Zari kwenye tangazo fulani akamtumia Babu Tale, sasa mimi niliiona nikwambia Tale huyu jamaa ana kitu cha kufanya tumute tumuelekeze tunataka tufanye hivyo, tukamuita tukafanya, hadi unaona hiyo video imekamilika ni miezi mitatu,” Madee ameiambia Planet Bongo ya EA Radio na kuongeza.

“Hiki kitu ina gharama kuliko hata video ya kawaida kuna mmoja nilimfuata muhindi aliniambia kila sekunde moja laki nikapiga hesabu nikaona ni milioni kama 16, nikaona siwezi kufanya nikarudi nikakaa na mchizi nikamuelewesha akanipa bajeti ya kawaida,” amesema.

Ameongeza kuwa licha kuoneka sura ya Jacqueline Wolper katika video hiyo hapakuwa na mazungumzo kati yao bali walimuweka tu.

No comments:

Post a Comment