Mwaka jana 2016 mtandao wa Youtube ulitoa taarifa kuwa utaboresha programu yake ili kuwapa urahisi watumiaji wake kushare video moja kwa moja wakiwa kwenye mtandao huo na kuchat live kwa video watakayokuwa wameishare.
Habari nzuri ni kwamba tayari huduma hiyo imeshaingia barani Afrika kwa watumiaji wote wa Android na iOS ambapo sasa unaweza kufanya vitu vyote kupitia App yako ya YouTube.
Je, utashare na utachati vipi ukiwa kwenye mtandao huo maarufu zaidi duniani? Njia ya kwanza hakikisha ume-update programu yako ya Youtube.
Ukimaliza ku-update juu ya App kuna kitufe kimeongezwa cha Share bonyeza hapo kisha utakuta sehemu ya View Contacts bonyeza hapo kwa ajili ya kuongeza majina ya watu ambao utahitaji kushare na kuchati nao kuhusu video utakayoishare.
Hatua ya mwisho chukua link ya video uipendayo kisha iweke kwenye uwanja na hapo utaanza kuchati na ndugu jamaa na marafiki uliyowaalika.Tazama maelekezo vizuri kwenye video hapo chini (Video by TECH WORLD)
Awali maboresho haya yalianza kwa nchi za bara la Amerika ya Kaskazini mapema mwaka huu kabla ya kufika barani Ulaya na Afrika.
Maboresho haya huenda yakawasaidia wasanii na watu wengine wanaotumia mtandao huo kuwa karibu na mashabiki wao kwani watakuwa na uwezo wa kuchati moja kwa moja na watazamaji wake tofauti na zamani ambapo walikuwa wanasoma maoni pekee.
No comments:
Post a Comment