Mpaka sasa unatakiwa kufahamu kwamba Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya dhamana yaliyowasilishwa na Mfanyabiashara Yusuf Manji ambae anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.
Hata hivyo kabla ya kutupiliwa maombi hayo, Manji alisimama na kuieleza Mahakama kwamba ameamua kukataa kuendelea kuwakilishwa na Wakili Peter Kibatala kwa sababu za kisiasa.
Manji amedai alipopeleka maombi ya dhamana Mahakamani hapo alimpa maelekezo wakili Joseph Tedayo lakini alishangaa kesi ilipofika Mahakamani kwa ajili ya kisikilizwa maombi yake, akawakilishwa na wakili Peter Kibatala.
No comments:
Post a Comment