Breaking




Tuesday, 8 August 2017

SERIKALI YAZIKATAA ZILE TAKWIMU ZILIZOSEMA CLOUDS TV NA RADIO NDIO ZINAZOSIKILIZWA ZAIDI NCHINI





Serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)  imejitokeza mbele ya vyombo vya habari na kutoa taarifa ya kupinga tafiti zilizotolewa na kampuni ya GeoPoll na kueleza kuwa tafiti hizo sio takwimu rasmi (Official Statistics) kwa kuwa  hukusanywa kwa mfumo ambao hautambuliwi na Ofisi hiyo ya Taifa ya Takwimu.

Akizungumza juu ya tukio hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa amebainisha kuwa,  Ofisi yake inapenda kujulisha umma kuwa takwimu hizo za Geo Poll sio rasmi na hazikufuata mfumo unaotambuliwa na Ofisi yake hapa nchini huku ikikiuka kifungu cha 20 cha Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015.

“Takwimu hizi sio sahihi na sio rasmi. Tunapenda kujulisha umma juu ya hilo. Hivyo takwimu za GeoPoll sio sahihi na waache mara moja na wafuate taratibu na vigezo vilivyowekwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu. Suala la takwimu sio kama mtu anaenda kukata majani shambani, zinautaratibu wake wa kuzikusanya tunataka wafuate utaratibu  zilizowekwa.” Ameeleza Dk. Albina Chuwa

Zaidi soma taarifa hii hapa chini


No comments:

Post a Comment