Breaking




Sunday, 13 August 2017

OBAMA,RAIS MAGUFULI KUHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA UHURU KENYATTA




 

Na Karim Mtila 

Rais wa awamu iliyopita  wa Marekani,Barack Obama ni miongoni mwa wageni wa heshima waliotajwa kualikwa kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta.

Kamati ya kiapo inyoongozwa na mwanasheria mkuu wa Kenya,Joseph Kinyua imesema tayari imekamilisha kuandaa orodha ya viongozi watakaoalikwa kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais Kenyata kama matokeo hayo hayatafanikiwa kupingwa mahakamani.

Viongozi wa Afrika ambao wanatarajiwa kualikwa kwenye sherehe hizo ni Paul Kagame(Rwanda),Yowel Mseven (Uganda),John Pombe Magufuli (Tanzania),Jacob Zuma(Afrika kusini), na Rais wa Nigeria Muhammed Buhari.

Viongozi kutoka ulaya watakaopewa  mualiko ni pamoja na Chansela wa Ujerumani Bi Angel Markel na waziri mkuu wa Uingereza,Theresa May.

Wengine ni Tajiri wa Afrika,Aliko Dangote,Rais wa China Xi jinping na waziri mkuu wa zamani wa Italia, Matteo Renzi.

"Tunanadaa sherehe za kuapishwa Rais ambazo zitafuata muongozo wa katiba,orodha inajumuisha Rafiki wa Rais ,viongozi wa Afrika na viongozi wengine mbalimbali Duniani" Alisema mmoja wa wanachama wa kamatiya mandalizi

kwa mujibu wa sheria za Kenya,sherehe za kuapishwa zitafanyika siku 14 baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi ili kuvipa nafasi vyama vingine vilivyoshindwa kufanya maamuzi juu ya matokeo hayo.

Theresa May. 
Read more at: https://www.standardmedia.co.ke/article/2001251128/barack-obama-invited-for-uhuru-s-swearing-in-ceremony

Theresa May. 
Read more at: https://www.standardmedia.co.ke/article/2001251128/barack-obama-invited-for-uhuru-s-swearing-in-ceremony

No comments:

Post a Comment