Breaking




Tuesday, 15 August 2017

RAIS MAGUFULI AHAMISHA UWANJA




Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) Dodoma ilitenga Ekari 143 zilizopo Nara Barabara ya Singida nje kidogo ya mji wa Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa uwanja na kituo cha michezo kitakachojengwa kwa msaada wa serikali ya Morocco.

Waziri wa Habari, Mwakyembe amesema kuwa Rais Magufuli alitoa oda ya uwanja huo kuhamishwa na kupelekwa maeneo yaliyo karibu na mji wa Dodoma ili kutoa fursa kwa vijana na watoto kutumia uwanja huo pindi utakapokamilika kwani sehemu ambayo ilitengwa awali ni mbali sana kutoka mjini Dodoma.

"Tunamshukuru sana Rais wetu wa Tanzania Magufuli kwa kuikumbuka sekta ya michezo kwa kuomba Morrocco watujengee eneo changamani, walio wengi wanafikiri ni kiwanja cha mpira wa miguu lakini hapana hili ni eneo changamani litakuwa na michezo ya aina yote, mwanzoni kama mnakumbuka tulipata eneo Nara eneo kubwa tu tuliomba ekari 150 tulipewa lakini Mhe. Rais Magufuli aliona kuna umbali kutoka Dodoma mjini mpaka Nara zaidi ya kilomita 70 akaona siyo rafiki, yeye angependa kuona vijana wake wa shule ya msingi na sekondari wakitoka shule wanakimbia uwanjani na umbali usiwe kikwazo" alisema Mwakyembe

Aidha Mwakyembe anadai kuwa Rais Magufuli aliagiza litafutwe eneo lingine
"Rais Magufuli aliagiza litafutwe eneo karibu na Dodoma mjini tujenge hiyo 'stadium' na kwa bahati nzuri sana agizo la Rais lilitekelezwa, tunamshukuru sana Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuhakikisha tunapata eneo zuri kuelekea Dar es Salaam karibu na Nane Nane linaitwa Zuguni ambapo sasa tumepata ekari 300 na hizo zote tunazihitaji kwa sababu tunataka eneo hili changamani liwe la mfano katika ujenzi wa viwanja Tanzania kwa sababu tunataka baadaye kuwa na hoteli, kuwe na hosteli kwa vijana, tuwe na majumba makubwa ya michezo" alisisitiza Mwakyembe

Waandisi, wabunifu na wataalam wa udongo kutoka nchini Morocco wameingia nchini Tanzania kufanya ziara na tathmini juu ya ujenzi wa eneo hilo changamani Dodoma

No comments:

Post a Comment