Serikali ya DR Congo imetoa amri ya kusitishwa kwa mitandao yote ya kijamii ili kuzuia usambazaji wa picha na video za ghasia zinzoendelea katika kanda hiyo .
Aidha hatua hiyo imechukuliwa kufuatia ongezeko la upinzani dhidi ya rais Joseph Kabila ambaye amekataa kujiondoa madarakani wakati awamu yake inamalizika mwezi Desemba .
Migomo ya kitaifa imepangwa kufanyika Jumanne na Jumatano .
Mapigano ya Jumatatu baina ya kundi la Bundu dia Kongo na vikosi vyaa usalama ,lilipelekea vifo vya watu 14 kutokea .
Mkuu wa idara ya mawasiliano nchini humo Oscar Manikunda Musata amefahamisha kwamba mitandao ya kijamii kama Twitter,Whatsap ,Facebook na Instagram itafungwa kwa muda .
No comments:
Post a Comment