WAKAZI wa kijiji cha Chamtunda, wilaya ya Kibiti mkoani Pwani wametakiwa kuchukuwa tahadhari kwa kuyafanyia usafi maeneo yanayowazunguka, ikiwamo kunywa maji safi na salama, ili kuepuka kupata magonjwa ya kuhara ambayo yamekikumba kijiji hicho na kuua watu wawili.
Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Khatibu Chaulembo katika kikao cha robo mwaka cha baraza la madiwani.
"Ugonjwa wa matumbo umeingia katika kijiji cha Chamtunda na kusababisha watu 42 kuugua matumbo huku watu wawili wakipoteza maisha, inatakiwa wanchi kuchukuwa taadhari ili msipate ugonjwa huo," alisema.
Pia aliongeza kuwa wilaya hiyo inatarajia kujenga vituo vya afya saba ambapo mapato ya ndani na bajeti fedha zake zitatumika katika kujenga vituo hivyo.
No comments:
Post a Comment