TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kanda ya kati inamshikilia aliyekuwa akigombea nafasi ya uwakilishi kanda namba 8 Yono Stanley.
Mgombea huyo aliyekuwa akiwania nafasi ya kuwakilisha mikoa ya Ruvuma na Njombe anashikiliwa na kuhojiwa na taasisi hiyo akidaiwa kutaka kutoa rushwa kwa wajumbe ili wamchague kinyume na sheria.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Ramadhan Mambosasa alisema kuwa mgombea huyo alikutwa na jumla ya Sh 500,000 kwenye chumba cha kujisaidia (choo) ambacho kipo nje ya ukumbi wa uchaguzi.
Kamanda huyo alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa amezigawa na kuhifadhi Sh.50,000 kwenye kila bahasha . "Ni kweli anashikiliwa na kuhojiwa na Takukuru kwa tuhuma za kutaka kutoa rushwa," alisema Mambosasa.
No comments:
Post a Comment