Kiungo Papy Kabamba Tshishimbi tayari yuko nchini na ameungana na wenzake visiwani Zanzibar kwa ajili ya kambi.
Yanga imepita Unguja ikiwa njiani kwenda Pemba ambako itaweka kambo yake kabla ya kuivaa Simba wikiendi ijayo katika mechi ya Kombe la Shirikisho.
Siku chache zilizopita, Yanga walitangaza kupoteza mawasiliano ya Tshishimbi raia wa DR Congo aliyekuwa anakipiga Mbabane Swallows ya Swaziland.
Lakini baadaye, taarifa zinaeleza walimpata na ametua nchini tayari kusaini mkataba na kumalizana na Yanga.
Mmoja wa viongozi wa Yanga amesema, Tshishimbi ataanza mazoezi mjini Pemba na mara ya kwanza ataonekana katika mechi dhidi ya Simba kuwania Ngao ya Jamii.
No comments:
Post a Comment