Breaking




Sunday 8 October 2017

KINGINE CHAIBAMIZA MAREKANI

Sungo blog

Kimbunga Nate, cha ngazi ya 1, kimepiga pwani ya Marekani siku ya Jumamosi usiku. Majimbo manne yanayotarajiwa kukabiliwa na kimbunga hicho, Louisiana, Mississippi, Alabama na Florida, walikuwa wamechukua hatua muhimu ili kuzuia uharibifu, baada ya kimbunga Harvey, Irma na Maria kusababisha uharibifu mkubwa katika majimbo hayo.

Wataalamu wa hali ya hewa hakutarajia kutokea siku ya Jumamosi ka kimbunga chenye nguvu kuliko vile vitatu vilivyotangulia ambavyo vilisababisha uharibifu mkubwa katikamajimbo ya Texas, Florida na Puerto Rico. Kimbunga Nate kilikua tayari kimepoteza nguvu kilipofikia pwani ya Marekani. Mvua na upepo bado vinawatia wasiwasi viongozi wa majimbo manne yanayotihiwa.

Wakazi wa kutoka jamii nyingi wametakiwa kuhama, lakini wengi wamekataa kufuata maagizo ya polisi. Katika mji wa New Orleans, ambapo wakazi wa mij huo bado wana kumbukumbu ya kimbunga Katrina, na wana wasiwasi ya kutokea hasara kubwa kufuatia kimbunga Nate. "Tunahama tu iwapo kwa kimbunga cha nagazi ya 3," mkazi mmoja amesema.

Amri ya kutotoka nje

Siku ya Jumamosi alasiri, mji wa Bourbon Street ulikua umefurikwa na watalii.

Meya wa mji huo, Mitch Landrieu, hata hivyo aliweka muda wa kutotembea kuanzia saa 1 jioni Jumamosi hadi saa 1 asubuhi Jumapili na amewahimiza wananchi wenzake kuwa tayari. "Tumesha kumbwa na matukio kama haya. Hakuna sababu ya kuwa na hofu. Tunawahimiza wakazi kufanya kila wanachoweza ili kujiandalia tukio hilo: Mnapaswa kuwa na mpango. Mnapaswa kuwa tayari kulinda mali zenu binafsi, "Bw. Landrieu ameonya.

No comments:

Post a Comment