Breaking




Sunday 8 October 2017

UTEUZI KATIBU WA BUNGE WAZUA JAMBO

Sungo blog



Uteuzi wa katibu mpya wa Bunge umestua wakosoaji ambao wanadai utaratibu haukufuatwa kama kanuni zinavyotaka.

Jana, Rais John Magufuli alimteua Steven Kagaigai kuwa katibu mpya kushika nafasi ya Dk Thomas Kashililla ambaye atapangiwa kazi nyingine, lakini muda mfupi baada ya uteuzi huo kukaibuka mjadala.

Mbunge wa Kaliua (CUF), Magdalena Sakaya alisema anashangazwa na uteuzi huo kwa sababu hakukuwa na kikao cha kupendekeza majina matatu kwa Rais ili afanye ueuzi kama kanuni zinavyotaka.

Alisema yeye ni kamishna wa Tume ya Bunge ambayo hupendekeza majina hayo, lakini hajasikia kikao, tetesi, wala kufahamishwa kwa namna yoyote ile kama kuna uteuzi wa aina hiyo.

“Sijui kwa kweli nimesikia suala hilo kutoka kwako. Uwih!! Umefanyika uteuzi, kwa kweli hatujakaa na wala sijasikia,” alisema Sakaya.

Akilizungumzia suala hilo mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe alisema Rais hakufuata sheria katika kuteua.

Alisema Sheria ya Utawala wa Bunge inataka Rais kuteua Katibu wa Bunge kutoka kwenye orodha ya watu watatu ambao wamependekezwa na Tume ya Huduma za Bunge.

Lakini akasema Rais Magufuli ameteua bila ya mchakato huo kufanyika, kitu ambacho kinaonyesha Bunge limedhibitiwa.

No comments:

Post a Comment