sungo blog
Nairobi, Kenya. Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto amemaliza kupiga kura nakuielezea siku ya leo Alhamisi ni yenyefuraha kubwa kwa vile wananchi wa Kenyawatatekeleza moja ya vipengele vilivyomokwenye katiba ya nchi.
“Nimepiga kura yangu kwa uhuru na amani nasiku ya leo ni yenye furaha kubwa kwaniwananchi wanashiriki katika uchaguzi kwaamani ili kuipata serikali itakayowaleteamaendeleo,” amesema Ruto wakatiakizungumza na waandishi wa habari.
Ruto, ambaye ni mgombea mwenza wa RaisUhuru Kenyatta amepiga kura yake katikakituo cha Shule ya Msingi ya Kosachei eneola Turbo mjini Eldoret Magharibi mwa Kenya.
Soma: Polisi waingilia kati kulinda amani
Ruto amesema baada ya uchaguzi huo kukamilika wananchi wa Kenya wanapaswa kuanza kushughulika na mambo yanayohusu maendeleo yao na kuicha Serikali itakayochanguliwa kuzitatua kero zao.
“Tumekuwa na kampeni katika kipindi cha mwaka mzima sasa tuanze kutilia mkazo mambo yanayohusu wananchi...wananchi wana changamoto zinazohusu barabara, maji na mambo mengine hivyo macho yetu tuyapeleke huko, “ amesema.







No comments:
Post a Comment