Breaking




Thursday, 26 October 2017

YAANGUKANDEGE ILIYOBEBA WATALII SERENGETI


Sungo blog

Ndege ya Kampuni ya Coastal Aviation iliyobeba watalii 10 imeanguka na kujeruhiwatalii wawili na rubani ilipokuwa ikituakatika uwanja wa Lobo ndani ya Hifadhi yaTaifa ya Serengeti.

 Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, William Mwakilema amesema ajalihiyo imetokea jana Jumatano Oktoba25,2017 saa tisa alasiri ilipokuwa ikitua.

Amesema taarifa za awali zinasema chanzocha ajali hiyo ni mvua kubwa iliyokuwaikinyesha iliyosababisha uwanja kujaa maji.

Mwakilema amesema wakati rubani akituandipo ndege ilianguka na kusababisha wataliihao wawili kujeruhiwa.

“Waliojeruhiwa ni wawili na rubani ambaowalipelekwa jijini Arusha na baadaye Nairobikwa matibabuWengine walikuwa namaumivu kidogo ambao walipatiwa hudumana daktari wetu na baadaye wakasafirishwakwenda Arusha,” amesema.

 

Amesema wanashukuru katika tukio hilondege haikuungua na kwambailipokuwaikiserereka iligonga mti na kusimama.

Mhifadhi huyo amesema mbele kulikuwa na mawe, hivyo ingeyagonga na kulipuka ingesababisha madhara makubwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Mohamed Jafari hajapatikana ili kuzungumzia tukio hilo.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu amesema wanaendelea kulifuatilia na kwamba, wanasubiri taarifa kutoka kwa vyombo vya uchunguzi.



No comments:

Post a Comment