Breaking




Monday 9 October 2017

MOJA YA VITU VINAVYOTUGHARIMU WABONGO NI UJANJA UJANJA KWENYE BIASHARA

Sungo blog

Jana nilicheki taarifa ya Wanunuzi wa Korosho wakilalamika kwamba Wakulima huweka mawe na sijui mavitu gan ili kuongeza uzito.



Haya pia hufanyika kwenye Pamba kwa kuweka mbolea ya chumvi chumvi ili kuongeza uzito 

Haya pia hufanyika kwenye kahawa.

Bado hujaenda kwenye Mchele unauziwa mchele wa Morogoro kwa jina mchele wa mbeya.

Niliona kipindi fulani kule Tanga yanachumwa machungwa mabichi kabisa halafu yanawashiwa moto unao babua ganda la juu na kuwa la njano.

Kwa kifupi huko nje wanatujua sana kwa sifa za ujanja ujanja na jii hupelekea uaminifu kuisha.

Dunia ya sasa ni ya ushindani sana sasa baadae Watu wakiagiza bidhaa toka nje watu wanaanza kulia

No comments:

Post a Comment