Breaking




Wednesday, 4 October 2017

TAHADHARI YATOLEWA KWA WATAUGONJWAWTAUNINZANIA JUU 


 Sungoblog

Wizara ya Afya imetoa tahadhari kuhusukuwepo ugonjwa wa tauni katika nchi ya Madagascar ulioibuka Agosti.

Imeelezwa kuwa, kati ya wagonjwa 104walioripotiwa, 20 wamefariki dunia.

Taarifa iliyotolewa jana Jumanne na OfisaHabari wa wizara hiyo, Catherine Sunguraimesema Shirika la Afya Duniani (WHO)limeeleza nchini Madagascar mikoa minane imeripoti kuwepo wagonjwa ukiwemo mjimkuu wa nchi hiyo, Antananarivo.

Ugonjwa huo ulianza kuripotiwa Agosti 23hadi Septemba 28.

“Wengi walioripotiwa wameonyesha kuwa nauhusiano kwa njia moja au nyingine namgonjwa wa kwanza jambo linalothibitishayapo maambukizi ya ugonjwa wa tauni kati yabinadamu na binadamuHivyokwa mujibuwa WHO, ipo hatari ya wastani (moderate risk) ya ugonjwa huo kusambaa katika nchijirani na Madagascar,” imesema taarifa hiyo.

Wizara imesema tahadhari hiyo inatolewakwa kuzingatia kwamba, Madagascar haikombali sana na Tanzania na inawezekanakukawa na mwingiliano kati ya wananchi wanchi hizi mbili.

“Serikali inasisitiza kuwa mpaka sasaugonjwa wa tauni haujaingia nchiniKwakuwa magonjwa hayaangalii mipaka,tunahitaji kuchukua tahadhari madhubuti ilikuzuia ugonjwa huu usiingie nchiniHivyo,wananchi wanahimizwa kuzingatia kanuni zaafya za kuzuia ugonjwa huu, pia wanatakiwakuripoti haraka kwenye vituo vya huduma za afya waonapo dalili zozote za ugonjwa huu,” imesema wizara.

Sungura amesema hatua zilizochukuliwa baada ya kupata taarifa ya tahadhari ya WHO Septemba 29 ni kusambaza barua za tahadhari ya ugonjwa huo kwa makatibu tawala wa mikoa yote ya Tanzania Bara.

Makatibu tawala katika barua hizo wametakiwa kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa katika viwanja vya ndege, mipakani na bandari ili kubaini wagonjwa waingiao nchini wakiwa na dalili za ugonjwa huo

“Kupitia kwa waganga wakuu wa mikoa na wilaya, wizara inatoa maelekezo ya kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji na utambuzi wa magonjwa katika vituo vya kutolea huduma,” amesema.

Pia, wizara itatoa elimu kwa jamii kuhusu ugonjwa huo.

Kuhusu tauni

Ugonjwa huu husababishwa na bakteria anayejulikana kitaalamu “Yersinia pestis” ambaye hupatikana katika baadhi ya wanyama wadogo kama vile panya, paka, mbwa na viroboto.

Taarifa hiyo imezitaja njia kuu tatu ambazo mtu anaweza kupata maambukizi kuwa ni kung’atwa na viroboto vyenye maambukizi ya bakteria hao kutoka kwa wanyama kama vile mbwa na paka ambao huweza kubeba viroboto

“Kugusana bila kuwa na kinga mwili na majimaji yenye vimelea vya bakteria kutoka kwa mtu/mnyama aliyeathirika kwa njia ya kugusa sehemu zenye vimelea zilizochafuliwa na mgonjwa/mnyama na kisha mtu huyo kujigusa mdomoni au puani,” imesema taarifa hiyo.

Njia nyingine ni kugusana na majimaji yanayotoka kwa mgonjwa kwa njia ya kukohoa au kupiga chafya bila ya mgonjwa kufunika pua au mdomo.

No comments:

Post a Comment