Breaking




Wednesday 4 October 2017

MAREKANI YAWAFUKUZA WANADIPLOMASIA 15 WA CUBA

Sungo blog

Marekani yawafukuza wanadiplomasia 15 wa Cuba

Marekani imewafukuza wanadiplomaisa 15 wa Cuba ikisema kwa Cuba ilistahii kuwalinda wanadiplomasia wa Marekani kutokana mashambulizi ya kutumia sauti.

Waziri wa mambo ya kigeni nchini Cuba Bruno Rodriguez ameitaja hatua hiyo ya Marekani kuwa isiyokubalika.

Hatua hiyo ya wizara ya mambo ya kigeni inafuatia hatua ya Marekani ya kuwaondoa zaidi ya nusu ya wanadiplomasia wake kutoka mji mkuu wa Cuba.

Karibu watu 20 raia wa Marekani wamepatwa na matatizo ya kiafya mjini humo.

Nao wanadiplomasia wa Cuba wamepewa muda wa siku saba kuondoka Marekani.

Takriban watu 21 wanaofanya kazi kwenye ubalozi wa Marekani nchini Cuba wamelalamikia matatizo ya kiafya yakiwemo kupoteza uwezo wa kusikia na kisungusungu.

Ripoti za awali zinasema kuwa mashambulizi ya kutumia sauti ndiyo yalichangia.

Cuba imekana kuwalenga wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani na Marekani yenyewe haijailaumu serikali ya Cuba kwa mashambulizi hayo.

No comments:

Post a Comment