Breaking




Tuesday, 13 February 2018

KESI ZA MADAI YA TALAKAZAONGEZEK


Sungo blog


Kesi 1,218 za madai ya talaka visiwaniZanzibar zimeripotiwa katika mahakamambalimbali za kadhi kuanzia Januari hadiDesemba, 2017.

Naibu Waziri wa Nchi Afisi ya RaisKatiba,Sheria na Utumishi wa Umma na Utawalabora, Khamis Juma Maalim amesema hayoleo Februari 13, 2018 katika kikao cha Barazala Wawakilishi wakati akijibu swali lamwakilishi wa Konde, Omar Seif Abeid.

Katika swali lake, Abeid alihoji sababu zandoa nyingi hasa za vijana kudumu mudafupihuku akitaka kujua katika kipindi chamwaka 2017 ni madai mangapi ya ndoayamefikishwa katika mahakama ya kadhi ilikupatiwa ufumbuzi.

Katika majibu yake Maalim amesemakiwango cha kesi hizo ni nyingi ukilinganishana mwaka 2016 ambapo kulikuwa na kesi1,000.

Amesema katika kesi za mwaka 2017,  kesi884 ziliripotiwa katika mahakama za kadhi zaUnguja,  440 zimetolewa uamuzi na 444 badozinaendelea kusikilizwa katika mahakamahizo kwa hatua zaidi za kisheria.

Amesema kwa upande wa Pemba, kulikuwana  kesi 334, kati ya hizo 249 zimetolewauamuzi huku 85 zikiendelea kusikilizwa.

Kuhusu sababu za ndoa kuvunjika katikakipindi cha muda mfupi sambamba nakuwekwa sheria ya kuzuia utoaji talaka,Maalim amesema swali hilo ni zuri lakini ningumu kwa sababu jambo hilo litakwendakinyume na maadili ya Wazanzibar walio wengi ambao ni Waislam.

“Kama tunavyoelewa wananchi wengi wa Zanzibar ni Waislam ni wazi kuwa kuandaa kwa Sheria kama hiyo ni kwenda kinyume na Sheria zilizowekwa na dini ya kiislam,” amesema,

“Hatuna utafiti ambao unaonyesha kuwa kati ya mwanamke na mwanaume nani ni sababu ya kutoka kwa talaka hovyo ijapokuwa suala la talaka ni la siku nyingi.”

Amesema kazi kubwa inayofanywa na wizara yake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ni utoaji wa elimu juu ya kuishi vema katika maisha ya ndoa, lengo ni kuona suala la talaka linapungua kwa kiasi kikubwa.

No comments:

Post a Comment