Breaking




Monday, 12 February 2018

NCHI HII IMEFIKA SEHEMU YA HOVYO SANA -MSIGWA

Sungo blog


Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini (CHADEMA), Peter Msigwa amefunguka na kudai nchi ya Tanzania imefika mahali pa hovyo kutokanana watawala kuiendesha nchi kwa mtazamowao na sio kufuata sheria na kanuni zilizopo.

Msigwa ametoa kauli hiyo wakati alipokuwaakimuombea ridhaa mgombea Ubunge Jimbola Kinondoni Salum Mwalimu ili aweze kupatakura za ndio kwa wananchi hao siku yakupiga kura ambapo mgeni rasmi katika haflahiyo alikuwa Waziri Mkuu mstaafu naMjumbe wa Kamati Kuu CHADEMAMhe. Edward Lowassa , huku akisindikizwa namameya na Wabunge mbalimbali kutokaUKAWA.

"Watawala wanaendesha nchi kwa'personality' na badala ya sheria na kanuni.Kwa bahati mbaya sana wale ambaowanategemewa kusemakukemea pamoja nakuonya wamekaa kimyaLakini baadhi yetutumeamua iwe mvuajuaiwe mabomu yapolisivituo vya polisi hata gerezatutazungumza hatutoogopa mtu yeyote",amesema Msigwa.

Pamoja na hayoMsigwa ameendelea kwakusema "nchi ya Tanzania imefika mahali ambako kiongozi hawezi kusemwa, Mkuu wa Mkoa hata Spika wa Bunge".

Kwa upande mwingine, Msigwa amewaambia wananchi wa Jimbo la Kinondoni kwamba wakimuona Mbunge anajikomba komba serikalini basi watambue mtu huyo hatambui wajibu wake anaopaswa kuutekeleza au kuufanya.

No comments:

Post a Comment