Breaking




Tuesday 6 March 2018

DC CHIWAMBA AKABIDHI BAISKELI 40 KWA WALEMAVU WA VIUNGO

Sungo blog


Mkuu wa wilaya ya Liwale Mhe.Sarah Chiwamba (wa pili kushoto) na mbele (kulia) ni watu wenye ulemavu wa viungo wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi baiskeli 40 kwa walemavu wa viongo iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya maendeleo ya jamii wilayani Liwale mkoani Lindi. 

Walemavu wenye ulemavu wa viungo katika wilaya ya Liwale mkoani Lindi  wamepatiwa msaada wa vifaa wezeshi (Baiskeli) kwa lengo la kuwasaidia katika shughuli zao na mahitaji mengine kama binadamu wengine

Hafla hiyo ya kukabidhi baiskeli hizo kwa walemavu hao ilifanyika katika viwanja vya ofisi ya maendeleo ya jamii wilayani Liwale march 3 huku wahisani wa zoezi hilo wakiwa ni TAWICO ambao waliwezesha msaada wa  baiskeli 40.

Awali wakati wa ufunguzi Mh; Sarah Chiwamba mkuu wa wilaya ya Liwale aliwashukuru TAWICO kwa kutoa msaada wa baiskeli 40 kwa walemavu na kusema kuwa  walemavu watamudu kuendelea na harakati zao za kila siku kwa ufanisi kwakuwa  usafiri wa basikeli  utawawezesha kurahisisha kazi zao za kila siku.

 Mkuu wa wilaya huyo aliwaambia walemavu na wananchi waliohudhurio hafla hiyo kuwa “ msaada huu mnaojionea leo (march 3)  ni faida za utunzaji wa maliasili zetu hivyo tuendelee kwa pamoja kutunza maliasili zetu  ili tupate tija zaidi.

Pia amewataka  walemavu  kuridhika, kushukuru na kuthamini baiskeli walizopewa kwa kukuzitunza ili ziweze kuwasaidia kwenye utendaji wao wa shughuli zao za kila siku.

Kwa upande wao baadhi ya walemavu ambao wamepatiwa baiskeli hizo walijawa na furaha zisizo na kifani kwani kwa kupatiwa msaada huo na kusema kuwa baiskeli hizo zitarahisisha katika shughuli zao za kiuntendaji  za kila siku.

Hata hivyo baadhi ya wazazi  ambao walikuwepo kwenye hafla hiyo wakiwa na watoto wao  wakielezea maisha ya watoto wao yalivyokuwa kabla ya kupatiwa baiskeli hizo na hadha waliokuwa wakipata na kusema kuwa msaada huo utakuwa na tija kwao.

Kwa upande wake Namsifu Marwa ambaye ni  mhifadhi mkuu  kanda ya kusini mashariki selous  ameeleza sababu hasa iliyopelekea wao kuja kutoa msaada huo wa baiskeli katika wilaya ya Liwale  amesema kuwa ni kuongeza hari ya utunzaji shirikishi wa maliasili na vile vile mhifadhi alitumia nafasi hiyo kuwashauri wananchi wa Liwale kuanzisha miradi  rafiki ya mazinira ikiwemo ufuaji wa nyuki, samaki na kuanzisha ranchi za jamii

No comments:

Post a Comment