Breaking




Wednesday 14 March 2018

RAILA ODINGA AWATAKA WAFUASI WA CHAMA CHAKE KUUNGA MKONO MAJADILIANO YA UHURU

Sungo blog

Nairobi, Kenya. Kiongozi wa ODM, Raila Odinga amewaomba wabunge kutoka chama chake kuunga mkono majadiliano yaliyofikiwa katika kikao cha Ijumaa kati yake na Rais Uhuru Kenyatta.

Odinga aliwataka wabunge hao wasiyumbishwe na watu waliojipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Aliwaambia wabunge wa chama hicho kwamba mkutano uliofanyika kwenye Ofisi za Rais zilizoko Jengo la Harambee Ijumaa iliyopita ni matokeo ya tukio la Januari 30 ambapo Raila aliapa kama rais wa watu.

Aliwahimiza kutumia kikamilifu fursa ya mpango uliofikiwa ili kuhakikisha mazungumzo ya kitaifa yanaanza.

"Mnapaswa kuunga mkono mazungumzo ya kitaifa kwa sababu ni zao la kuapa kwetu," alisema Raila wakati wa mkutano uliofanyika katika Jengo la Orange Jumanne.

Kijembe
Katika kile kilichoonekana kuwa ni kijembe kilicholengwa kuwafikia vinara wa muungano wa Nasa, Raila alisema: "Ni kile kiapo ndicho kimezaa juhudi za kuelekea mazungumzo ya kitaifa. Mlikuwa wapi Januari 30 kabla ya kuanza kutuuliza maswali? "

Aliwaambia wabunge kuwa mabadiliko ya mwelekeo yalikuwa muhimu ikiwa chama hicho kinataka kunufaika na ushindani wa siasa siku zijazo.

"Hatutafika popote ikiwa tutajiingiza katika ukinzani ambao tumekuwa tukishiriki kipindi cha miaka mitano iliyopita. Tutakosa mengi na tunaweza tusiwe madhubuti katika kushinikiza mageuzi kwa sababu tutakuwa tunapiga porojo badala ya kusemezana."

Raila alizungumzia hata mvutano uliosababisha mgawanyiko wa upinzani ndani ya Bunge wakati wanachama wengine wa Nasa walipigania nafasi za uongozi zilizotengwa kwa ajili ya wapinzani.

Ili kuonyesha dhamiri yake kwa mkutano kati ya Rais Kenyatta na Raila, chama hicho kiliandamana hoja ya kutafuta msaada wa mabunge yotw mawili ili kupitisha ajenda yenye hatua tisa ambazo viongozi wawili hao walikubaliana baada ya mkutano wao wa Ijumaa iliyopita.

No comments:

Post a Comment