Breaking




Thursday 15 March 2018

RAIS MAGUFULI ASISITIZA WATANZANIA KUDUMISHA AMANI

Sungo blog

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa mtu akichezea amani ya nchi amechezea maisha yake.

Rais Magufuli leo Machi 15, 2018 wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza sigara cha Philips Moris International mjini Morogoro.

“Ukichezea amani unachezea maisha yako. Unaweza ukadhani wewe uko mbali ukafikiri haitakupata. Isipokupata wewe, itampata hata ndugu yako,” amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo Rais amezungumzia mashamba yanayofutwa ameeleza kuwa “Nilishasema mashamba yote yanayofutwa, wapewe wananchi bure, ni mali yao, walidhulumiwa tangu zamani kwa wakubwa fulani fulani kujimilikisha”.

No comments:

Post a Comment