Hali ya usafiri barabara ya Kilwa jijini Dar esSalaam leo asubuhi Machi 13, 2018 si shwarikutokana na uhaba wa mabasi ya abiria.
Vituo vingi vya daladala kutoka Mbagala hadikatikati ya Jiji vimekuwa na idadi kubwa yaabiria wakisubiri usafiri kuanzia saa 12asubuhi.
Katika kituo cha Mbagala Rangi Tatu haliilikuwa mbaya zaidi kutokana na kuwepo kwaabiria wengi wanaotoka pembezoni mwaviunga vya Mbagala.
"Nipo hapa tangu saa 12:30 na sijaliona garila Makumbusho hadi muda huu. Magari yamaeneo mengine kama Posta na Kariakooangalau yanakuja moja baada ya nusu saa, ilahizi ruti ndefu hakuna kitu," amesemaAbdallah Lihende.
Naye Irene Gerars aliyekuwa kwenye kituocha Mbagala Zakhiem amesema, "nimetokakituo cha Rangi Tatu nimekuja huku angalaunipande gari la Buguruni nizunguke nalonikaunganishe la Ubungo mbele ya safari,lakini tangu nifike hapa ni zaidi ya dakika 45sijaliona gari la Buguruni hata moja.”
Mwandishi wa MCL Digital ameshuhudiavituo vya Kipati, Kizuiani, Misheni na AziziAlly ambavyo ni nadra kuwa na abiria wengiwa kwenda na kurudi Mbagala vikiwa vimejaaabiria.
No comments:
Post a Comment