MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa Misimu mitatu mfululizo Yanga ambayo imeweka kambi Mkoani morogoro kujiandaa na msimu mpya wa ligi Kuu Tanzania Bara leo asubuhi Agosti 2,2017 imetoa kipigo cha Mbwa mwizi baada ya kuinyuka timu ya Moro Kids bao 5-0 huku Donald Ngoma akifunga bao 2.
lkumbukwe Mwaka jana kipindi kama hiki Simba nao waliweka kambi mkoani Morogoro na kucheza mchezo wa kirafiki na timu hiyo ya Moro Kids ambapo simba ilifungwa bao 2-0 kutoka kwa timu hiyo inayomilikiwa na Taasisi ya kukuza na kuibua Vipaji ya Moro Youth.
Taasisi hiyo kwa sasa inaongoza kwa kutengeneza wachezaji wengi wanaowika katika timu kubwa zikiwemo Simba na yanga.
Baadhi ya wachezaji walioibuliwa na Taasisi hiyo ni pamoja na Hassani Kessy na Juma Abdul ‘Yanga’ ambao leo waliongoza kikosi cha yanga kuitandika timu yao hiyo ya zamani bao hizo 5.
Wengine ni Shiza Kichuya, Ally Shomari, na Shomari Kapombe’Simba’ Christopher Edward Kagera Sugar na Hemde Mau Azam.
Licha ya kupokea kichapo hicho Vijana hao wa Moro Kids walionesha upinzani mkali kwa Yanga kiasi cha kumshangaza kocha wa Yanga George Lwandamina na kuomba mchezo huo uchezwe vipindi vitatu, dakika 135 kwa lengo la kocha huyo kuchezesha timu tatu ambapo timu ya kwanza iliyoongozwa na Ngoma ilishinda bao 2-0 na timu ya Pili iliyoongozwa na Nahodha Canavaro ilishinda bao 1-0 na timu ya tatu mchanganyiko ilishinda bao 2-0.
Akizungumza baada ya kupokea kichapo hicho mmoja wa makocha wa Moro Kids Majutoa alisema.
“ Hiki ni kikosi chetu cha pili watoto wa chini ya miaka 17 kile kikosi chetu cha kwanza watoto chini ya miaka 20 kilichoifunga Simba Mwaka jana leo jioni kinamchezo wa Ndondo Cup Uwanja wa Saba Saba zidi ya Chicago ya Wagogo sababu nyingine wenzetu wameingia timu tatu kwa dakika hizo 135 sisi tuliingiza timu moja hata hivyo kama ulivyoshuhudia tumewapa upinzania mkali kama wanataka kesho kutwa tuludiane tukiwa kamili waone moto wetu”alisema Majuto
No comments:
Post a Comment