Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu kama ‘Mzee wa Upako’ amefunguka kuwa yeye ni moja ya Wachungaji ambao wapo nyuma sana kwenye mitandao ya kijamii na kukiri kuwahi kuibiwa kwenye mtandao wa Facebook na watu wanaotumia jina lake.
Mzee wa Upako amesema kutokana na kuwa na elimu ndogo ya mitandao ya kijamii amewahi kuibiwa na watu mitandaoni waliokuwa wanawatapeli waumini wake kwa kutumia jina lake na kuwaomba watu hela.
“Nina akaunti ya Instagram na nimewafuata watu wanne tuu Magufuli, Jakaya, BBC na vyombo vingine vya habari….(kuhusu Facebook) kule niliibiwa sana kuna watu walikuwa wanatumia jina langu wanajiita Mzee wa Upako na kuwachangisha watu pesa,” amesema Mch. Antony Lusekelo kwenye mahojiano yake na kipindi cha Chomoza cha Clouds TV.
Hata hivyo Mzee wa Upako amesema kwa sasa kwenye simu yake hakuna hata Group moja la WhatsApp huku akidai kuwa wingi wa simu za kawaida zinazoingia ndiyo unamfanya asijiunge na makundi hayo kwani yanamaliza chaji.
No comments:
Post a Comment