Breaking




Wednesday 5 July 2017

Simba Wapanga Kuweka Kambi Afrika Kusini Kujiandaa na Ligi Kuu..!!!

KIKOSI cha Simba kinatarajiwa kuanza mazoezi leo huku pia kikipanga kwenda kuweka kambi Afrika Kusini kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/18 utakaoanza Agosti mwaka huu.

Uamuzi wa uwanja ambao utatumika kufanya mazoezi hayo ulitarajiwa kujulikana jana jioni katika kikao cha kamati ya utendaji ya klabu hiyo.

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa pia kocha mkuu wa timu hiyo, Mcameroon Joseph Omog, anatarajiwa kurejea nchini Jumamosi kwa ajili ya kuendelea na majukumu yake.

"Timu itaanza mazoezi kesho (leo), na safari ya kwenda kambini Afrika Kusini itajulikana baada ya wachezaji wote waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao kukamilika," kilisema chanzo chetu.

Taarifa zaidi zilieleza kuwa kikao cha jana pia kilitarajiwa kujadili mchakato wa usajili wa wachezaji wao ambao wataitumikia klabu hiyo katika msimu ujao na mashindano ya kimataifa.

"Kikao kitajadili na kufanya uamuzi kulingana na mazingira yaliyopo, lakini masuala ya ufundi yatazingatia sana ushauri wa kocha na benchi nzima la ufundi," kiliongeza chanzo hicho.

Maandalizi ya Tamasha la Simba Day ambalo huwa linafanyika Agosti 8 kila mwaka nayo yatajadiliwa katika kikao hicho kitakachoongozwa kwa mara ya kwanza na Kaimu Rais, Salim Abdallah na Iddi Kajuna

No comments:

Post a Comment