Breaking




Wednesday, 5 July 2017

Serikali ya Afrika Kusini kujitoa ICC?

Rais Omar al Bashir amekuwa kiongozi wa Sudan tangu mapinduzi ya mwaka 1989Haki miliki ya pichaAP
Image captionRais Omar al Bashir amekuwa kiongozi wa Sudan tangu mapinduzi ya mwaka 1989
Chama tawala nchini Afrika kusini kimeonesha kuwa bado kina mipango ya kuiondoa Afrika kusini kwenye uanachama na Mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC.
ICC inatarajia kutangaza siku ya alhamisi kama Afrika Kusini ilivunja sheria kwa kushindwa kumkamata Rais wa Sudan Omar al Bashir, alipoitembelea nchi hiyo mwaka 2015.
Rais Bashir anashutumiwa kutekeleza mauaji ya kimbari wakati wa mzozo wa Darfur.
Serikali ya Afrika kusini ilikua na mipango hiyo tangu miaka miwili iliyopita.
Ilikua ni msukumo uliofanywa na baadhi ya serikali za Afrika dhidi ya taasisi hiyo zikidai kuwa ICC imekua ikilionea bara la Afrika na viongozi wake.
Mahakama kuu nchini Afrika Kusini yenyewe imesema serikali imekua ikifanya mchakato huo kinyume na katiba, ikishindwa kulipeleka suala hilo bungeni.
Pamoja na hayo chama cha ANC kimesema hakitarudu nyuma, wataendelea na mipango yao ya kujiondoa ICC.

No comments:

Post a Comment