Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara amesema atawashughulikia Maafisa Elimu wa shule za msingi na sekondari ambao watashindwa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waratibu wa elimu na walimu wakuu walevi wanaosababisha utoro wa walimu shuleni.
Dkt. Ntara amesema hayo akiwa mjini Tabora wakati wa kikao cha watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nzega walipokuwa wakijitathimini utendaji wao katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita ili waweze kujipanga kwa ajili ya mwaka huu wa fedha.
Amesema kuwa wakuu wa shule ambao ni walevi wamesababisha kushuka kwa nidhamu baina ya walimu na wanafunzi kwa sababu muda mwingi wanafunzi wanakaa darasani bila walimu wa kuwasaidia na kuwafundisha na hivyo kujikuta wakijihusisha na mambo maovu.
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara
Dkt. Ntara alisema hali hiyo imesababisha katika baadhi ya Shule kufanya karibu nusu ya walimu kutokuwepo kazini , hali inayowasababisha baadhi ya wanafunzi wa kike kujikikuta wakijihusha kimapenzi na walimu au watu wazima jambo linalowapelekea kupata ujauzito wangali wadogo.
"Nikipata habari ya kuwepo kwa mkuu wa shule ambaye ni mlevi tena wakati wa kazi na hajachukuliwa hatua za kisheria, nitaanza kuwachukulia hatua Maofisa Elimu awe wa shule ya msingi au sekondari kwa kushindwa kusimama katika nafasi zenu" alisema RAS
No comments:
Post a Comment