Wachezaji wa Arsenal wakishangilia kwa pamoja wakiwa na Ngao ya Jamii kwa kuifunga Chelsea kwa penalti 4-1 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 90.
Mabingwa wa Kombe la FA, Arsenal wametwaa Ngao ya Jamii kwa kuifunga Chelsea kwa penalti 4-1 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 90.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Wembley, Arsenal ikiwa na mshambuliaji wake mpya, Alexandre Lacazette, ilianza kwa kasi lakini hadi mapumziko hakuna timu iliyoweza kupata bao.
Chelsea ilifanikiwa kupata bao dakika ya 46 mfungaji akiwa Victor Moses aliyetumia makosa ya mabeki wa Arsenal walioshindwa kuzuia mpira wa kona.
Wachezaji wa Arsenal wakishangilia.
Bao hilo la Chelsea lilidumu hadi dakika ya 80 ambapo Arsenal walisawazisha kupitia kwa Saed Kolasinac aliyefunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa faulo.
Faulo hiyo ilitokana na faulo aliyochezewa Mohamed Elneny na Pedro wa Chelsea ambaye alitolewa kwa kadi nyekundu na mwamuzi Bobby Madley katika dakika ya 80. Baada ya dakika 90, mwamuzi aliamuru penalti zipigwe ambapo Arsenal walishinda 4-1.
Wakiendelea kushangilia kwa pamoja.
Waliokosa penalti kwa Chelsea ni kipa Thibaut Courtois na Alvaro Morata huku Gary Cahill akifunga. Waliofunga penalti za Arsenal ni Theo Walcott, Nacho Monreal, Alex Oxlade-Chamberlain na Olivier Giroud.
No comments:
Post a Comment