Katika matumbo yetu kuna kemikali asidi ijulikanayo kama Hydrochloric acid. Asidi hii husaidia katika umeng’enywaji wa vyakula, husaidia kuua vijidudu tulivyokula pamoja na chakula na pia husaidia kuweka mazingira ya asidi zingine katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi vizuri.
Kukiwa na hitilafu katika uzalishwaji wake kunaweza kuzalishwa kwa wingi zaidi na kiasi huweza kubadilika na kuwa katika mfumo wa hewa (gesi) ambayo hujaa tumboni na kuweza kupanda hadi kwenye njia ya juu ya chakula na kufika kooni.
Kwa hiyo, kiungulia na tumbo kujaa gesi hutokana na matatizo katika uzalishwaji na ufanyaji kazi wa asidi hii ya tumboni mwetu.
Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kusababisha au kuongeza uzalishwaji wa asidi nyingi tumboni na kuweza kupelekea au kuongeza matatizo ya kiungulia na tumbo kujaa gesi.
Maambukizi ya bakteria wajulikanao kama Helicobacter pylori ambao husababisha vidonda vya tumbo
Saratani (Kansa) kwenye tumbo au utumbo
Kula chakula kingi
Baadhi ya vyakula na viungo kama vile vyakula vya mafuta mengi, vyakula vilivyokaangwa, nyanya, vitunguu, matunda jamii ya machungwa/machenza, vitunguu swaumu nk
Maziwa na bidhaa zitokanazo na maziwa
Kafeini (Kama kwenye kahawa, soda, chai nk)
Msongo
Uvutaji wa sigarakiungulia 1
Pombe
Uzito mkubwa na uzito uliopitiliza
Tiba:
Cha msingi sana ni kujua kitu gani kinasababisha tatizo hilo kwako na kisha kuanza kuacha na kukiepuka kabisa.
Kama ni magonjwa basi kwanza yadhibitiwe vizuri ili asidi isizidi kuzalishwa zaidi, kama ni vyakula na vinywaji basi ni vyema kuviepuka.
Kuna dawa nzuri kabisa zipo ambazo ni mahususi kwa ajili ya kupunguza uzalishwaji wa asidi hiyo au kupunguza asidi ambayo tayari imeshazalishwa. Mifano ya dawa hizo ni M
No comments:
Post a Comment