Akizungunza kwa njia ya simu Mkuu wa Mkoa wa Dar Paul Makonda amesitisha zoezi la kuondoa Tinted kwenye magari zoezi ambalo lingeanza kesho.
Makonda amesema kwamba baadhi ya watu huweka tinted kwenye magari kwa ajili ya ulinzi wa vifaa na vitu ndani ya gari kupunguza majaribu ya watu kuviona na kuiba.
Akatolea mfano wanawake wanaoendesha magari halafu yuko peke yake kwenye gari uwezekano wa kufuatiliwa na majambazi ni mkubwa hivyo tinted husaidia kupunguza watu wa nje ya gari kuona idadi ya watu waliomo ndani ya gari.
Pia amesema magari ya mikoani yanatumika katika kusafiri kuja Dar sasa inabidi anapoingia Dar aidha apaki gari mpakani kuepuka kukamatwa na sakata la gari yake kuwa na tinted au kutokutumia magari hayo kuja Dar kitu ambacho Makonda amesema si sahihi maana mtu kanunua gari limsaidie kusafiri.
RC Makonda amesitisha zoezi hilo mpaka hapo jeshi la polisi litakapompatia maelezo ya kutosha.
Pia amesisitiza bado jeshi la pollisi lina uwezo wa kudhibiti wahalifu wachache wanaotumia magari ya vioo vya tinted kufanya uhalifu.
Zaidi msikilizie hapa chini
No comments:
Post a Comment