Polisi nchini Hispania wamesema wanawake 13 waliokuwa wamelazimishwa kufanya kazi za ukahaba katika kituo kimoja cha utalii mjini Puerto Banus wameachiliwa huru.
Wanawake hao wanadhaniwa kuwa waliletwa katika eneo hilo, kutoka nchini Bulgaria.
Polisi katika nchi zote mbili wamewakamata watu 34, wanaotuhumiwa kuwatishia wanawake hao na familia zao kuwafanyia fujo iwapo watakataaa kufanya kazi hiyo.
Kukamatwa kwa watu hao, kumekuja takriban miaka mitatu baada ya polisi kutahadharishwa kuhusiana na mtandao wa Ukahaba na wanawake ambaye alikwepa mtego wa kuingizwa katika biashara hiyo.
Polisi wanasema wanawake hao pia wamekuwa wakitumika kuibia wateja wake hao na kwamba baadhi yao walikuwa wakitumia madawa ya kulevya.
No comments:
Post a Comment