Sungo blog
Madaktari nchini Nigeria wameanza mgomo wa kutofanya kazi na kufunga mahospitali yote baada ya madai kuwa serikali imeshindwa kukidhi mahitaji yao.
Kwa mujibu wa habari,madaktari hao wameitaka serikali kukidhi mahitaji yao kama walivyokubaliana hapo awali.
Kati ya makubaliano serikali iliyoweka na madaktari hapo awali ni kulipa mishahara yao ya nyuma,kuimarisha sekta ya afya nchini humo,na vilevile kuwapandisha vyeo madaktari wanaostahili.
Ripoti zinaonyesha kuwa baadhi ya makubaliano kati ya serikali ya Nigeria na madaktari wake yaliwekwa toka utawala wa rais Olusegun Obasanjo na Goodluck Jonathan.
Hata hivyo mgomo huo unazidi kuuchafulia jina uongozi wa rais Buhari kwani tayari kuna migomo ya walimu wa chuo na kadhalika inayozidi kuendelea nchini humo.
No comments:
Post a Comment