Saturday, 2 September 2017

BI HINDU KUZIKWA LEO

Sungo blog




Naibu Katibu Mkuu wa CUF, upande waProfesa Ibrahim Lipumba, Magdalena Sakaya amesema chama hicho kimepokea kwa masikitiko kifo cha Mbunge mteule wa Viti Maalum Hindu Mwenda

Hindu alifariki dunia ghafla juzinyumbani kwake Kibada Kigamboni na anatarajiwa kuzikwa leo saa 7 mchana katika makaburi ya Kisutu wilayani Ilala,  Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza, jana Jumamosi Septemba 2 Sakaya amesema  Hindu alikuwa ni mpambanaji  na mtu mwenye kukijenga chama hicho  kuanzia miaka ya 90  hivyo ni pigo kubwa kuondoka kwake.

‘’Hata ukifika  Tabora leo hii hakuna mwanachama wa CUF asiyemjua Hindu’ ’amesema Sakaya.

“Sijui niseme nini maana zilikuwa zimebaki siku chache tu aende Dodoma kuapishwa baada ya kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) mwezi uliopita,” amesema Sakaya ambaye pia ni Mbunge wa Kaliua Tabora.

No comments:

Post a Comment